Sisi kama watafiti katika tasnia ya falsafa ya maadili na kisiasa. Kazi yetu imejikita katika mitazamo tofautitofauti ya kifalsafa, na ni nadra sana kujikuta tukikubaliana kitamzamo sisi kwa sisi. Hata ivyo, tunakubaliana juu ya umuhimu wa mabadiliko ya kina katika uhusiano wetu na wanyama wengine. Na tunalaani matendo yote yanayohusisha kuwatendea wanyama kama vitu au bidhaa.
Kwakadiri yanavyohusisha vurugu na madhara yasiyo ya lazima, tunatangaza kwamba unyanyasaji wa wanyama si wa haki na hauwezi kutetewa kimaadili.
Katika etholojia na neurobiolojia, imethibitishwa kuwa mamalia, ndege, samaki, na wanyama wengi wasio na uti wa mgongo wana hisia – yaani, uwezo wa kujisikia furaha, maumivu na hisia. Wanyama hawa ni viumbe wenye ufahamu; wana mtazamo wao kuhusu ulimwengu unaowazunguka. Inamaana kwamba wana maslahi: tabia zetu huathiri ustawi wao na zinaweza kuwafaidi au kuwadhuru. Tunapojeruhi mbwa au nguruwe, tunapoweka kuku au salmon katika vizuizi, tunapomchinja ndama kwa ajili ya nyama yake au mink kwa ajili ya ngozi yake, tunakiuka kabisa masilahi yao ya kimsingi.
Kimsingi, madhara haya yote yanaweza kuepukwa. Inawezekana kabisa kujiepusha na kuvaa ngozi, kuhudhuria matamasha ya mapigano ya mafahali na rodeo, au kuwaonyesha watoto simba waliofungwa kwenye hifadhi za wanyama. Wengi wetu tunaweza tayari kuishi bila vyakula vitokanavyo na wanyama na bado tuna afya, na maendeleo ya baadaye ya uchumi wa vegan itafanya mambo kuwa rahisi zaidi. Kwa mtazamo wa kisiasa na kitaasisi, inawezekana kuacha kuwaona wanyama kama rasilimali.
Kwamba viumbe hawa si wa spishi (kundi) ya Homo sapiens haina msingi kimaadili: Japokuwa inawezekana kufikiri kiurahisi kwamba maslahi ya wanyama yapo chini ukilinganisha na maslahi yawanadamu, mtazamo huu wa kibaguzi wa kibaologia hauna msingi wa kutosha na unaweza kushindwa kirahisi. Kila kitu kingine kuwa sawa, utofauti wa kibiologia kati ya viumbe (iwe umetokana na aina ya spishi (kundi), rangi ya ngozi, au jinsia) hauwezi kutumika kuhalalisha kutendewa kusiko kwa usawa.
Kuna tofauti kati ya wanadamu na wanyama wengine, kama vile ilivyo kwamba kuna utofauti ndani ya viumbe wa kundi moja. Ni kweli kwamba, baadhi ya uwezo wa juu wa utambuzi unaweza kupelekea kuibuka kwa maslahi ya aina fulani, ambayo yanaweza kutumika kuhalalisha upendeleo fulani. Lakini uwezo wa kutunga symphonies, kufanya mahesabu ya juu ya hisabati, au kufikiria kuhusu yajayo, japokuwa yana maana, ayawezi kuathiri kuzingatiwa ubora wa maslahi ya kiumbe wa kupata raha na kuepuka mateso. Maslahi ya wenye akili zaidi miongoni mwetu hayana umuhimu zaidi ya maslahi sawa ya wasio na akili. Kusema vinginevyo kunaweza kuwaweka watu binafsi katika madaraja ambavyo hayana msingi kimaadili. Mtazamo kama huo wa uwezo hauwezi kutetewa kimaadili.
Kwa hiyo ni vigumu kuepuka hitimisho hili: kwa sababu inadhuru wanyama bila lazima, unyanyasaji wa wanyama kimsingi sio haki. Kwa hivyo ni muhimu kufanya kazi kuelekea kutokomezwa kwake, haswa kwa kulenga kufungwa kwa machinjio, kupiga marufuku uvuvi, na kuendeleza mifumo ya chakula inayotokana na mimea. Ni ukweli usiopingika; mradi kama huo hautafikiwa kwa muda mfupi. Zaidi hasa, inahitaji kuachana na tabia za kibaguzi za spishi zilizokita mizizi na kubadilisha misingi ya taasisi nyingi. Hata hivyo, tunaamini, kwamba mwisho wa manyanyaso ya wanyama ndio upeo wa ushirikiano wa kipekee ambao ni wa kweli na wa haki kwa wasio wanadamu.
Ikiwa wewe ni mwanafalsafa wa kimaadili au kisiasa unaweza kuweka saini yako hapa.
বাংলা, عربي, dansk, Esperanto, français, Deutsch, English, Ελληνικά, Italiano, Português, Русский, español, Türkçe, Slovenščina